Mateka wa Mwisho Wakombolewe

Category:

Description

Watu wageni walikuwa wameivamia nchi. Waliingia na vishawishi vitamu kama peremende na kuwabembeleza hata wanaume wenye uwezo na kisha kuwashika mateka kama watumwa. Walikuwa wanafunganishwa kama ng’ombe dume ambao wanatayarishwa kulima shamba. Hawa wageni walitumia
mbinu nyingi kuwashika mateka wao. Wakati wingine walitumia ushawishi na ahadi za vitu vizuri katika nchi zao.

Mara nyingine walitumia nguvu za kinyama na kisha kuwachukua wakiwa wamefungwa shingo kwa shingo na kamba au minyororo hadi melini zilizowangojea baharini na kuwasafirisha mpaka nchi za mbali wakiwa nusu uchi huku wakiwa wamefungwa na minyororo.

Mwandishi alifanya kazi kama mtosha kodi na shirika la kutoza kodi kwa miaka 33, kisha akafungua kampuni yake ya ushauri wa kodi na baadaye kuanzisha kampuni ya utoaji vitabu ya Gideon Wisdom Publishers ambayo anaitumia kuandika vitabu.

Bwana Nyakiongora ni mtu wa familia, msomaji dhati wa vitabu, mwangalizi wa makini wa mambo ya siasa na shabiki wa mchezo wa kandanda. Zaidi ya hayo yote anampenda na kumcha Mungu na ujishugulisha na mambo ya ukristo na ushirikiano. Hiki kitabu cha”Mateka wa mwisho wakombolewe”
ni fumbo la maneno kuhusu Kenya na Africa na hata ulimwengu katika nyakati za historia, mamboleo na siku za usoni na washiriki kuweka kiwango cha juu cha uadilifu na huruma kwa binadamu wote.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mateka wa Mwisho Wakombolewe”

Your email address will not be published. Required fields are marked *